SERIKALI YA POKOT MAGHARIBI YATAKIWA KUELEZA HATIMA YA WANAFUNZI WANAOSOMEA NJE YA KAUNTI HII KUHUSU SWALA LA BASARI.

Na Benson Aswani
Baadhi ya wazazi katika kaunti hii ya Pokot magharibi wamelalamikia kukosa fedha za basari kwa ajili ya karo ya wanao hasa wanaosomea nje ya kaunti hii ya Pokot magharibi licha ya kutuma maombi hayo kwa afisi husika.
Wazazi hao wamesema kuwa wanapitia wakati mgumu kupata karo ya kuwalipia wanao ambao wanaitwa katika shule zilizo nje ya kaunti hii ya Pokot magharibi licha awali kuwa na matumaini kuwa wangepata afueni kufuatia kuzinduliwa fedha hizo na gavana John Lonyangapuo.
Wazazi hao sasa wanamtaka gavana Lonyangapuo kueleza hatima ya wazazi ambao wanao wanaitwa katika shule zilizo nje ya kaunti hii ya Pokot magharibi baada ya kuelezwa kuwa fedha za basari zinatolewa tu kwa wanafunzi ambao wanasomea katika shule za kaunti hii.