SERIKALI YA POKOT MAGHARIBI YASUTWA KWA KUTELEKEZA HOSPITALI YA KAPENGURIA

.
Mwakilishi wadi maalum katika bunge la kaunti hii ya Pokot magharibi Elijah Kasheusheu ameendelea kuibua maswali kuhusu hali ya hospitali ya kapenguria.
Kasheusheu sasa amewasilisha ombi kwa kamati ya bunge la kaunti kuhusu afya analosema linanuia kuangazia kwa undani hali ya hospitali hiyo na kubaini hatima yake kwa kile amedai kuwa imetelekezwa na uongozi wa kaunti hii.
Aidha Kasheusheu amemtaka waziri wa afya katika kaunti hii pamoja na maafisa katika wizara hiyo kufika mbele ya kamati hiyo kueleza ni kwa nini vifaa muhimu vya kuwahudumia wagonjwa havipo katika hospitali hiyo.
Amemshutumu gavana wa kaunti hii John Lonyangapuo kwa kile amesema kuwa amejihusisha na maswala mengine yasiyo na umuhimu mkubwa wakati huu huku wananchi wakiendelea kuhangaika kwa kukosa huduma zinazostahili za afya.