SERIKALI YA POKOT MAGHARIBI YASHUTUMIWA KWA UKARABATI WA BAJETI.


Huenda serikali ya kaunti hii ya Pokot magharibi ikakosa kupokea tena mgao unaotolewa kwa serikali za kaunti baada ya kubainika kuwa uongozi wa kaunti umekuwa ukikarabati bajeti yake.
Haya ni kwa mujibu wa seneta wa kaunti hii dkt Samwel Poghisio ambaye amedai kuwa fedha za kaunti zimekuwa zikitumika kwa maswala ya binafsi na uongozi wa kaunti hii hali anayosema imepelekea kuathirika kwa miradi ya maendeleo katika kaunti hii.
Hata hivyo dkt Poghisio amesema kuwa huenda kiwango fulani cha fedha kikatolewa iwapo serikali na wabunge katika bunge la kaunti hii wataweza kuelewana kuandaa bajeti ya ziada ya pili.
Dkt Poghisio ametumia fursa hiyo kuwahimiza wakazi wa kaunti hii kuwa makini katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti mwaka huu na kuwachagua viongozi ambao wataweza kulinda fedha za umma na kuhakikisha kuwa wananchi wananufaika kutokana na ugatuzi.