SERIKALI YA POKOT MAGHARIBI YASHUTUMIWA KWA KUTELEKEZA HOSPITALI YA KAPENGURIA


Idara za uchunguzi ikiwemo tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC na idara ya uchunguzi wa makosa ya jinai DCI zimetakiwa kuingilia katika kuchunguza matumizi ya fedha ambazo zinatengewa idara ya afya kaunti hii ya Pokot magharibi.
Ni wito wake mwakilishi wadi mteule Elijah Kasheusheu ambaye anadai huenda fedha hizo zinafujwa kutokana na kile anasema licha ya kutengewa fedha hali ya hospitali ya kapenguria imeendelea kudorora huku wagonjwa wakihangaika kwa kutopata huduma zinazostahili kufuatia ukosefu wa vifaa maalum.
Kasheusheu amesema licha ya wahudumu wa fya katika hospitali hiyo kuhatarisha maisha yao wakiwahudumia wagonjwa bila vifaa maalum vya kujilinda hasa kipindi hiki ambacho maambukizi ya virusi vya corona yameendelea kuongezeka, serikali ya kaunti imesalia kimya kuhusiana na swala hilo.