SERIKALI YA POKOT MAGHARIBI YASHUTUMIWA KWA KUKITHIRI UFISADI.


Aliyekuwa mshauri wa gavana wa kaunti hii ya Pokot magharibi kuhusu maswala ya siasa Stephen Kolemuk amepongeza juhudi za idara za kukabili ufisadi nchini kuhakikisha maafisa waliohusika katika ufisadi kaunti hii wanakabiliwa.
Akizungumza na wanahabari Kolemuk amesema kuwa ni wakati maafisa wote waliohusika katika kupora fedha ambazo zilinuiwa kutekeleza miradi ya kuwanufaisha wakazi wa kaunti hii kukabiliwa huku akiwataka maafisa hao kubeba msalaba wao.
Aidha Kolemuk ametaka kuendeshwa uchunguzi kuhusu baadhi ya miradi ambayo imetekelezwa eneo bunge la pokot kusini na baadhi ya maeneo kaunti hii ya pokot magharibi akidai imetumika kuendeleza ufisadi.
Wakati uo huo Kolemuk amependekeza kufanyika ukaguzi wa maisha kwa viongozi katika kaunti hii ya Pokot magharibi ili kubaini viwango vya mali waliyo nayo akisema wengi wao wanamiliki mali nyingi kinyume na mishahara wanayopata.