SERIKALI YA POKOT MAGHARIBI YASHUTUMIWA KWA KUKITHIRI UFISADI
Gavana wa kaunti hii ya Pokot magharibi John Lonyangapuo ameendelea kushutumiwa kufuatia madai ya matumizi mabaya ya fedha za umma katika serikali yake.
Akizungumza na kituo hiki mwakilishi wadi maalum wa Kapenguria ambaye pia ni mwanachama wa kamati ya bajeti katika bunge la kaunti hii Elijah Kasheusheu amedai kuwa zadi ya fedha milioni mbili, fedha za basari zimetolewa katika akaunti kinyume cha sheria.
Kasheusheu amemtaka gavana lonyangapuo kutosalia kimya kuhusiana hali hiyo na badala yake kuchukua hatua za kisheria dhidi ya maafisa waliohusika katika kupotea fedha hizo iwapo hakuhusika katika uovu huo.
Wakati uo huo kasheusheu ametoa wito kwa idara za uchunguzi ikiwemo tume ya kukabili ufisadi EACC pamoja na afisi ya DCI kuanzisha uchunguzi miongoni mwa maafisa wa serikali ya kaunti hii ya pokot magharibi ili kuwajibisha wote waliohusika kupotea fedha hizo.