SERIKALI YA POKOT MAGHARIBI YASHUTUMIWA KWA KUITELEKEZA IDARA YA AFYA.
Baadhi ya viongozi katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameendeleza shutuma zao dhidi ya uongozi wa kaunti hii kwa kile wanadai kuitelekeza hospitali ya Kapenguria.
Wakiongozwa na seneta Samwel Poghisio, viongozi hao wamaisuta serikali ya kaunti hii kwa matumizi mabaya ya fedha hali ambayo imepelekea ukosefu wa dawa na vifaa vya matibabu katika hospitali hiyo pamoja na upungufu wa madaktari.
Ni kauli ambayo pia imetolewa na mbunge wa kapenguria Samwel Moroto ambaye amesema kuwa wakazi wengi wanaotafuta huduma za matibabu wanalazimika kuelekea katika hospitali ya level 4 mjini kitale na ile ya rufaa ya Eldoret kutokana na uhaba wa dawa na vifaa vya matibabu katika hospitali ya Kapenguria.