SERIKALI YA POKOT MAGHARIBI YASHUTUMIWA KUFUATIA UHABA WA MAJI MJINI MAKUTANO.

Hisia mseto zimeendelea kuibuliwa miongoni mwa viongozi wa kaunti hii ya pokot magharibi kufuatia uhaba wa maji unaoshuhudiwa mjini makutano baada ya kampuni ya Kenya power kukata umeme katika eneo la kusambaza maji kufuatia deni inalodai serikali ya kaunti.
Mwakilishi wadi maalum Elijah kasheusheu ameitaka serikali ya kaunti hii kulipia deni hilo ili kuhakikisha wakazi mjini makutano wanapata maji ambayo ni muhimu zaidi hasa msimu huu wa janga la corona ambapo yanahitajika zaidi.
Hata hivyo mwakilishi wadi mteule wa eneo la lomut Nancy chombir amekosoa mbinu anayotumia kasheusheu kuwasilisha malalamishi yake akimtaka kutumia bunge na kukoma kuingiza siasa kwa kila maswala yanayohusu wananchi.