SERIKALI YA POKOT MAGHARIBI YAPOKEZWA VIFAA VYA KUKAGUA ARDHI KIDIJITALI.


Mwenyekiti wa kamati ya ardhi, nyumba na maendeleo ya miji katika bunge la kaunti hii ya Pokot magharibi Johnson Lokato amepongeza shirika la FAO pamoja na la umoja wa ulaya EU kwa kukabidhi kaunti hii vifaa vya kukagua ardhi kidijitali.
Lokato ambaye pia ni mwakilishi wadi ya Lelan amesema kuwa hatua hii itarahisisha shughuli za kukagua ardhi pamoja na kutoa hati miliki za ardhi kwa wakazi huduma ambazo zilikuwa zikipatikana tu mjini Eldoret.
Lokato ametumia fursa hiyo kuwahimiza wakazi wa kaunti hii ya pokot magharibi kutokuwa na hulka ya kuuza ardhi zao na badala yake kuzihifadhi kwanI zina manufaa makubwa.