SERIKALI YA POKOT MAGHARIBI YAPOKEZWA BIDHAA ZA KUKABILI UTAPIAMLO.


Serikali ya kaunti hii ya Pokot magharibi imepokezwa bidhaa za kukabili utapia mlo miongoni mwa watoto katika kaunti hii kutoka shirika la action against hunger kupitia mpango wa mother to mother boost.
Akizungumza wakati akipokezwa bidhaa hizo waziri wa afya kaunti hii Christine Apakoreng amesema bidhaa hizo zitasambazwa katika vituo mbali mbali vya afya ili kutolewa kwa watoto ambao wana uzani wa chini ikilinganishwa na umri wao.
Aidha apakoreng amesema kuwa utafiti wa hivi punde umeashiria visa vya utapia mlo vimeongoza katika kaunti hii hali ambayo imechangiwa pakubwa na athari za janga la corona pamoja na upungufu wa maziwa.
Kwa upande wake adfisa katika shirika hilo Salome Tsindori amesema kuwa bidhaa hizo za kima cha shilingi milioni 1.5 zitasaidia kaunti hii kwa kipindi cha miezi mitano.
Ameongeza kuwa shirika hilo linaendesha mafunzo kwa wahudumu mbali mbali wa afya ya jamii kaunti hii ambao watatoa matibabu kwa watoto walio na tatizo hilo la utapia mlo.