SERIKALI YA POKOT MAGHARIBI YAJITETEA KUHUSU MADAI YA KUTELEKEZA SEKTA YA AFYA

Serikali ya kaunti hii ya Pokot Magharibi imejitetea kutokana na madai ambayo yamekuwa yakiibuliwa na baadhi ya viongozi kuwa imeitelekeza idara ya afya hasa hospitali ya kapenguria.
Wakifika mbele ya kamati ya bunge la kaunti kuhusu afya, maafisa kutoka wizara ya afya na idara zingine husika kaunti hii wakiongozwa na waziri Christine Apakoreng, wamekiri kuwepo uhaba wa vifaa muhimu katika hospitali hiyo hali wanayosema imesababishwa na hitilafu ya mpangilio katika uagizaji, wakitoa hakikisho kuwa baadhi ya vifaa vitakuwa vikiwasili kufikia juma lijalo.
Abuya kuhusu swala la ukosefu wa ambulansi katika vituo vya afya, waziri wa afya kaunti hii christine Apakoreng amesema kuwa kwa jumla kaunti ina ambulansi 14 ila kwa sasa ni 7 pekee zinazohudumu kufuatia kutokuwa katika hali nzuri zingine saba swala analosema linashughulikiwa.
Apakoreng aidha maafisa hao wamepata wakati mgumu kuelezea kamati hiyo jinsi ambavyo fedha zilizotengwa kununua vifaa vya matibabu kutoka shirika la kusamabaza dawa na vifaa vya matibabu kemsa zilivyotumika wakionekana kujikanganya kuhusu kiwango halisi cha fedha ambazo zimetumika.

[wp_radio_player]