SERIKALI YA POKOT MAGHARIBI YAIMARISHA JUHUDI ZA KUKABILI MALARIA.


Serikali ya kaunti hii ya pokot magharibi kupitia wizara ya afya inatarajiwa kusambaza neti kwa wakazi ambao walijisajili katika juhudi za kukabali kusambaa ugonjwa wa malaria hasa msimu huu wa mvua kubwa ambayo inashuhudiwa kaunti hii.
Akizungumza baada ya kupokea neti hizo waziri wa afya kaunti hii Christine Apakoreng amesema kuwa serikali ya kaunti hii imepokea vifurushi alfu 5400 vya neti hizo ambapo kwa kila kifurushi kuna neti 40.
Apakoreng amesema kuwa neti hizo zitasambazwa katika hospitali za kila kaunti ndogo ambapo zitatolewa kwa watu alfu 821 kutoka nyumba alfu 126 waliojisajili kupokea neti hizo huku neti zingine zikitarajiwa kuwasili katika kaunti hii juma lijalo.