SERIKALI YA POKOT MAGHARIBI YAAPA KUIMARISHA ZAIDI KILIMO CHA MIFUGO.

Na Moses Ruto

Serikali ya kaunti hii ya Pokot magharibi imejitolea kuhakikisha kuwa inaimarisha kilimo hasa cha ufugaji ikiwa ndio tegemeo kubwa kwa wakazi wengi wa kaunti hii kuhakikisha kila mkazi ananufaika na kilimo hicho.
Akizungumza baada ya kupokea chakula cha mifugo kutoka kwa shirika la kilimo na chakula FAO kwa ushirikiana na NRT miongoni mwa mashirika mengine, gavana John Lonyangapuo amesema hadi kufikia sasa serikali yake imetekeleza miradi kadhaa ya kilimo ikiwemo wa unyunyiziaji maji mashamba, kuendeleza chanjo ya mifugo miongoni mwa mingine.
Wakati uo huo gavana Lonyangapuo amesema kuwa ataendelea kushirikiana na mashirika mbali mbali kuhakikisha kaunti hii inaimarika zaidi katika kilimo huku pia akitoa wito kwa wahisani zaidi kujitokeza ili kushirikiana na serikali yake katika kufanikisha juhudi hizo.