SERIKALI YA POKOT MAGHARIBI YAAHIDI KUWEKEZA KATIKA WATAALAM.
Serikali ya kaunti hii ya Pokot magharibi imetenga zaidi ya shilingi milioni 30 zitakazotumika kufadhili wakazi kutoka kaunti hii waliofuzu katika taaluma mbali mbali kuendeleza masomo katika mataifa ya nje.
Haya ni kulingana na gavana wa kaunti hii John Lonyangapuo ambaye aidha amesema kuwa kiwango hicho kitaongezwa lengo kuu likiwa kuhakikisha kaunti hii inapata wataalam waliofuzu katika Nyanja mbali mbali ili kuzuia hali ambapo inalazimika kutegemea huduma za wataalam kutoka nje ya kaunti hii.
Aidha Lonyangapuo amesema kuwa serikali yake itahakikisha wataalam watakaofadhiliwa na serikali ya kaunti hii watatoa huduma zao kwa wakazi wa kaunti hii katika kipindi ambacho serikali itaandikishana nao ili kuhakikisha huduma kwa wakazi zinaimarishwa hata zaidi.