SERIKALI YA LONYANGAPUO YAZIDI KUKASHIFIWA KWA MADAI YA UFISADI.


Uchaguzi mkuu wa agosti 9 unapokaribia wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kuwa makini na kuweka kwenye mizani kila kiongozi ili kuwachagua viongozi kulingana na rekodi yao ya maendeleo pamoja na wenye nia ya kuhakikisha maisha ya wakazi yanaimarika.
Aliyekuwa gavana wa kaunti hii Simon kachapin ambaye pia ametangaza nia ya kugombea tena kiti hicho katika uchaguzi wa mwezi agosti, ameendelea kuisuta serikali ya sasa kwa madai ya kutowajibika na kuhakikisha miradi inatekeleza kuimarisha maisha ya wakazi.
Kachapin amesema kuwa licha ya serikali yake kutengewa kiasi kidogo cha fedha ikilinganishwa na serikali ya sasa, alitekeleza na kuikamilisha miradi mingi katika kipindi chake cha uongozi, akidai hamna miradi ambayo imeanzishwa na kukamilishwa na uongozi wa gavana John Lonyangapuo.
Kachapin amedai kuwepo ufisadi ambao unaendelezwa na serikali ya gavana Lonyangapuo huku akizitaka idara za kuendeleza uchunguzi dhidi ya matumizi mabaya ya fedha kuharakisha uchunguzi dhidi ya seriaki ya kaunti hii ya Pokot magharibi.