SERIKALI YA KAUNTI YA TRANS NZOIA YATARAJIWA KUSAMBAZA NETI KWA WAKAZI.


Serikali ya kaunti ya Trans nzoia kupitia wizara ya afya inaendeleza uhamasisho kwa wadau katika maandalizi ya zoezi la kutoa neti kwa wakazi katika juhudi za kupunguza maradhi ya malaria katika kaunti hiyo.
Kulingana na waziri wa afya katika kaunti hiyo Clare Wanyama, serikali ya Trans nzoia itasambaza zaidi ya neti alfu 600 lengo kuu likiwa kupunguza visa hivyo hadi asilimia 75 kufikia mwaka 2023 akiongeza kuwa wizara yake inalenga kutoa matibabu kwa watakaoambukizwa ugonjwa huo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa maswala ya kukabili maambukizi ya malaria kaunti ya Trans nzoia Dkt Philip Bett amesema kila nyumba itapokea neti tatu na ambazo zitatumika kwa kipindi cha miaka mitatu.