SERIKALI YA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI YATEKELEZA UBOMOZI MJINI MAKUTANO


Mwakilishiwadi maalum katika kaunti ya Pokot Magharibi Ozil Kasheusheu ameukashifu vikali ubomoaji wa maduka mjini Makutano bila kuwapa wafanyabiashara hao notisi mapema.
Amemtaka gavana Prof. John Lonyangapuo kuelewana na wafanyabiashara hao badala ya kutumia maafisa wa polisi kuwakandamiza wafanyabismashara hao.
Mwakilishiwadi wa Kapenguria Maddy Polokow amewahimiza wakazi wote wa mji wa Kapenguria kutokubali kununua ploti kwenye mji bila kupata mwelekeo rasmi kutoka kwa wapangaji wa miji.
Hata hivyo mwakilishiwadi maalum Josephine Cheprum ameushabikia ubomoaji huku akimpongeza gavana Lonyangapuo kwa kutekeleza wajibu huo wa ubomoaji.
Amesema ubomoaji huo umefanyika kwa manufaa ya upangaji mzuri wa mji huku akiwarai viongozi kutoingiza siasa kwenye shughuli hiyo nzima.