SERIKALI YA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI KUEKEZA KATIKA SEKTA YA VIWANDA


Gavana wa kaunti hii ya Pokot Magharibi John Lonyang’apuo amesema kuwa serikali yake inanuia kuwekeza pakubwa katika sekta ya viwanda.
Akizungumza na wanahabari, Lonyang’apuo amesema kuwa mpango mzima wa kuafikia lengo hilo utaigharimu serikali yake zaidi ya shilingi milioni 200 ikiwa ni kwa mitambo pekee itakayotumika katika shughuli hiyo.
Lonyangapuo amesema viwanda hivyo vitahusu bidhaa zinazotokana na wanyama ikiwemo nyama, maziwa pamoja na ngozi.
Kadhalika Lonyang’apuo ameongeza kuwa lengo kuu la kuekeza kwenye sekta hiyo ni kujaribu kubinu nafasi za ajira miongoni mwa wakazi wa kaunti hii.