SERIKALI YA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI IMESHIRIKIANA NA KAMPUNI YA MKOPO YA APOLO ILIKUIMARISHA SHUGHULI YA KILIMO KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI


Wizara ya Kilimo ya kaunti hii ya Pokot Magharibi imetangaza rasmi ushirikiano na kampuni ya mkopo ya wakulima ya Apollo Agriculture ili kutatua shida za wakulima wa pokot magharibi hasa wapanzi wa mahindi
Akizungumza katika kikao na wanahabari mjini kapenguria, meneja wa upanuzi wa kampuni ya Apollo Paul Muthii, ametangaza ushirikiano huo huku akihoji kwamba nia ya ushirikiano huo ni kuhakikisha ongezeko ya mazao katika kaunti hii kwa kuhakikisha kwamba wakulima wa chini wanaweza kumudu bei ya pembejeo
Aidha, waziri kaimu wa wizara ya kilimo katika kaunti hii Thomas Wasike amesisitiza faida ya ushirikano huo kwa wakulima huku akiiomba kampuni ya Apollo kuangazia huduma zake hadi kwa wapanzi wa vitunguu katika wadi za Lomut na Batei na mazao mengine yanayopandwa katika kaunti hii