SERIKALI YA GAVANA LONYANGAPUO YALAUMIWA KUFUATIA KIFO CHA MWAKILISHI WADI YA LELAN.

Mbunge wa Kapenguria kaunti hii ya Pokot Magharibi Samwel Moroto amelaumu utepetevu wa serikali ya gavana John Lonyangapuo kufuatia kifo cha mwakilishi wadi ya Lelan Johnson Lokato.
Akizungumza na kituo hiki Moroto amesema kuwa huenda Lokato hangeaga dunia iwapo serikali ya gavana Lonyangapuo ingetilia maanani umuhimu wa kuimarisha sekta ya afya hasa kwa kuhakikisha huduma bora za matibabu katika hospitali ya Kapenguria.
Moroto amesema lokato alilazimika kutafuta huduma katika hospitali moja ya kibinafsi mjini makutano kutokana na hali duni ya hospitali ya Kapenguria ambapo alizidiwa na kuaga dunia.
Moroto amemshutumu gavana Lonyangapuo kwa kile amedai kupora fedha za umma kwa nia ya kuzitumia kuendesha kampeni za uchaguzi mkuu wa mwezi agosti hali ambayo imepelekea kudorora zaidi huduma katika hospitali ya Kapenguria.