SERIKALI YA BUSIA YASHIKILIA MSIMAMO WAKE WA KUTOWALIPA WAHUDUMU WA AFYA AMBAO WANAGOMA


Serikali ya kaunti ya Busia imeshikilia kwamba haitawalipa wahudumu wa afya ambao wanaendelea kushiriki mgomo na kulemaza huduma katika hospitali za uma kwenye kaunti hiyo.
Gavana wa kaunti hiyo Sospeter Ojamong’ akizungumza katika hospitali ya Busia baada ya kushiriki kikao na madaktari na wafanyikazi wa mahabara ili kuangazia mikakati ya kuboresha utendakazi amesema kuwa tayari maafisa wa serikali wametumwa kwenye hospitali tofauti za eneo hilo ili kubaini wahudumu wa afya ambao wamerejea kazini kufikia sasa.