SERIKALI YA BUNGOMA YASHUTUMIWA KWA KUTOTIMIZA AHADI YAKE KWA WAFANYIBIASHARA WADOGO WADOGO

Wanaharakati chini ya vuguvuvgu la Bungoma Liberation wameshutumu serikali ya kaunti ya Bungoma kwa kuendelea kuwatoza ada za juu wahudumu wa boda boda licha hali ngumu ya uchumi.
Vuguvugu hilo kupitia msemaji wake Isaiah Sakonyi limemkashifu gavana Wyclife Wangamati kwa kutotimiza ahadi yake ya kuwaondolea mzigo wa kodi wahudumu wa boda boda na wafanyibiasha wadogo wadogo.
Wahudumu wa boda boda katika kaunti hiyo ya Bungoma wamelalamikia kusahaulika na serikali ya Wangamati wakisema wanalazimika kulipa ushuru wa juu licha ya kazi kuwa chini hasa kipindi hiki kigumu cha janga la corona.