SERIKALI YA BARINGO KUBUNI MAHAKAMA YAKE.

Serikali ya kaunti ya Baringo imetangaza mikakati ya kubuni mahakama yake ya kaunti hiyo itakayosikiliza kesi mbalimbali zikiwemo za wanaokwepa kulipa ushuru.
Gavana Starnely Kiptis amesema mahakama hiyo itaanza kuhudumu mwakani baada ya kukamilika mchakato wa kutia sahihi mkataba wa maelewano na mahakama kuu ya kabarnet ambayo pia inatarajiwa kumtuma hakimu kuhudumu katika mahakama hiyo.
Wakati hayo yakijiri gavana kiptis pia amewagiza walinda usalama kukaza kama hata zaidi katika kukabiliana na pombe haramu kaunty hiyo.