SERIKALI KUWAKABILI WALIMU WANAOFANIKISHA UDANGANYIFU KWENYE MITIHANI YA KITAIFA


Naibu Kamishna wa kaunti hii ya Pokot Magharibi Kennedy Lunalo amegadhabishwa na kauli za wanafunzi wa shule za upili katika kaunti hii kwamba walimu wao hawajakuwa wakiwasaidia kuiba mtihani ili kufanya vizuri katika mitihani ya kitaifa kupitia udanganyifu.
Akizungumza wakati wa warsha iliyowakutanisha washikadau wa sekta ya elimu katika kaunti hii, Lunalo amesema kuwa serkali kamwe haitawavumilia walimu wanaofanikisha udanganyifu kwenye mitihani ya kitaifa akisema kufikia sasa mianya yote imezibwa.
Katika mkutano huo ulioitishwa na wizara ya elimu, changamoto zinazowakumba walimu na wanafunzi katika kaunti hii vilevile jinsi ya kuzikabili zilijadiliwa.
Lunalo kwa upande wake amewaagiza machifu na manaibu wao kuendelea kuwahamasisha wakaazi kuhusu umuhimu wa elimu na kuachana na utamaduni wa kuwakeketa watoto kike vilevile kuwaoza mapema.
Walimu, viongozi wa kijamii, viongozi wa kidini vilevile mashirika mbalimbali walihudhuria mkutano wenyewe.