SERIKALI KUU YATAKIWA KUIMARISHA USALAMA KATIKA MIPAKA YA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI


Serikali imetakiwa kuweka mikakati ya kuimarisha usalama katika mipaka ya kaunti hii ya Pokot Magharibi na kaunti jirani hasa Baringo, Turkana na Elgeyo Marakwet.
Wakiongozwa na Lomer Japheth, wakazi katika kaunti hii wamelalamikia ongezeko la utovu wa usalama katika maeneo ya mipaka katika siku za hivi karibuni hali ambayo imegharimu maisha ya wakazi wengi wa kaunti hii ya Pokot Magharibi.
Wakazi hao wamesema licha ya oparesheni ambazo zimekuwa zikiendelezwa katika kaunti hizi ili kutwaa silaha zinazomilikiwa kinyume cha sheria, wakazi wengi wameendelea kumiliki silaha hizo wakitaka serikali kuendeleza oparesheni hiyo kwa makini ili kutwaa silaha zote zilizo miongoni mwa wakazi.
Yanajiri haya baada viongozi kutoka kaunti hii ya Pokot Magharibi na wenzao kutoka kaunti jirani ya Elgeyo Marakwet kuandaa mkutano wa amani siku ya jumamosi katika eneo la Chesogon ambapo baadhi ya viongozi wakiongozwa na mwakilishi kina mama kaunti hii Lilian Tomitom walishutumu vikali serikali kwa kuwatelekeza wakazi wa eneo hili.