SERIKALI KUU YALAUMIWA KUCHELEWESHA FEDHA ZA KILIMO KAUNTI YA TRANS NZOIA


Gavana wa kaunti ya Trans Nzoia Patrick Khaemba ameilaumu serikali kuu kwa kile amesema imehujumu sekta ya kilimo kwa kufeli kufadhili sekta hiyo ambayo iko chini ya serikali za magatuzi.
Akizungumza eneo bunge la Cherang’ani, gavana Khaemba amedai serikali kuu imekosa kutoa fedha ambazo zilinuiwa kufadhili shughuli za kilimo katika serikali za magutuzi hali ambayo imepelekea sekta hiyo kudorora.
Wakati uo huo Khaemba amewaahidi wakulima katika kaunti hiyo kuwa serikali itawapiga jeki katika kutafuta soko kwa bidhaa zao, akiwataka kuzingatia pakubwa teknolojia mpya katika shughuli zao za ukulima.

[wp_radio_player]