SERIKALI KUU NA YA KAUNTI HII YA POKOT MAGHARIBI YASHAURIWA KUWEKEZA ZAIDI KATIKA MIUNDO MISINGI YA SHULE


Wito umetolewa kwa serikali ya kaunti hii ya Pokot Magharibi kwa ushirikiano na serikali ya kitaifa kuwekeza zaidi katika miundo msingi kwenye shule za kaunti hii.
Ni wito wake mwakilishi wadi ya Riwo David Alukulem ambaye amesema baadhi ya shule katika kaunti hii zimelazimika kujenga madarasa kwa kutumia udongo ili kushughulikia hali ya dharura.
Wakati uo huo Alukulem amesema wanafunzi wengi wa kike walikata tamaa na masomo na kulazimika kuolewa baada ya kufungwa shule kwa takriba miezi tisa mwaka jana kutokana na ujio wa janga la corona.
Hata hivyo amesema juhudi zinaendelezwa kupitia machifu na wazee wa mitaa kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kwenda shule katika wadi ya riwo wanaenda shule.