SERIKALI IMEOMBWA KUWEKA MIKAKATI YA KUKABILI UHABA WA CHAKULA


Na Benson Aswani
Pana haja ya serikali kuweka mikakati kukabiliana na uhaba wa chakula vijijini na hata shuleni
Ni wito ambao umetolewa na mwakilishi wadi ya bratabwa reuben chepsongol ambaye anakariri kwamba kipindi kirefu cha ukame kimewaathiri wakazi na hata mifugo jambo ambalo analitaka serikali kuchukulia kwa uzito
Akizungumza nje ya majengo ya bunge la kaunti ya baringo chepsongol pia ametoa wito kwa wizara ya kilimo kwa ushirikiano na idara ya utabiri wa hali ya hewa kutoa mafunzo kwa wakulima kuhusu misimu ya upanzi
Chepsongol aidha ametoa wito kwa serikali kuweka mpango wa kununua mifugo kutoka kwa wafugaji ukame unaposhuhudiwa kwani wamekuwa wakienda hasara baada ya mifugo kuangamia kwa kukosa malisho na maji