SERA YA ASILIMIA 100 YA WANAFUNZI WANAOJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA YAPELEKEA CHANGAMOTO KATIKA SHULE ZA UPILI.


Sera ya serikali kuhakikisha asilimia 100 ya wanafunzi ambao wanajiunga na kidato cha kwanza imepelekea ongezo kubwa la wanafunzi katika shule za upili hali ambayo pia imekuja na changamoto mbali mbali.
Haya ni kwa mujibu wa wadau katika sekta ya elimu kaunti hii ya Pokot magharibi ambao wamesema kuwa hatua hii imepekelea changamoto ya uhaba wa miundo msingi ya kutosheleza idadi ya wanafunzi wanaijiunga na shule za upili ikiwemo mabweni.
Samwel Kapelku ni mwalimu mkuu wa shule ya upili ya mseto ya Sebit.
Kapelku sasa anatoa wito kwa wahisani kujitokeza kusaidia katika ujenzi wa baadhi ya miundo msingi katika shule hiyo ili kuwawezesha wanafunzi kuendeleza shughuli zao za masomo katika mazingira salama.