SENETA WA POKOT MAGHARIBI AWAHIMIZA WENYEJI KUDUMISHA AMANI MSIMU HUU WA KRISIMASI


Wenyeji wa kaunty ya pokot magharibi wanaoishi mpakani mwa kaunty jirani ikiwemo turkana baringo na elgeyo marakwet wametakiwa msimu huu wa krisimasi kudumisha amani
Ndio kauli yake seneta wa kaunty hii ya pokot magharibi dkt samwel poghisio ambaye amewataka wenyeji wanaoishi mpakani kudumisha amani na kuepukana na maswala yanayoweza kuleta uhasama miongoni mwa majirani msimu huu.
Aidha poghisio amewataka wenyeji wanaposherehekea kuzingatia umbali wa mita moja ilikuepuka janga hili la corona.
Huku shule zikifunguliwa mwaka ujao januari tarehe nne poghisio amewataka wanafunzi kukumbuka kwamba wao ni wanafunzi na kwamba hawafai kushurehekea hadi wasahau kwamba shule zinafunguliwa mwaka kesho