SENETA WA POKOT MAGHARIBI ATAKA USALAMA KUIMARISHWA MPAKANI MWA POKOT NA MARAKWET
Seneta wa kaunti ya pokot magharibi daktari samuel poghisio amewakashifu vikali wajambazi wanoainiminika kutoka katika jamii ya marakwet ambao waliwajeruhi watu wawili kwa kuwapiga risasi siku mbili zilizopita katika eneo la chepkokogh kwenye kaunti ya pokot magharibi.
Poghisio ameitaka wizara ya usalama wa ndani kufanya juhudi za kuwatafuta na kuwachukulia hatua kali majambazi hao ambao wamewakosesha amani wakazi wanaoishi mipakani.
Ametumia fursa hiyo kumsuta gavana john lonyangapuo kwa kuendeleza miradi isiyokiwa na umuhimu kwa wakazi wa pokot huku hali ya afya katika kaunti hiyo ikizidi kidorora. Amemsisitizia kuimarisha sekta ya afya kwa kuitengea fedha za kutosha badala ya kuzitumia kwa kununua mbuzi, kuku, samaki na ng’ombe.
Aidha poghisio amesema serikali ya aliyekuwa gavana wa kwanza wa pokot simon kitalei kachapin ilifanikisha maendeleo mengi sana katika muhula wake ikilinganishwa na serikali ya gavana lonyangapuo ambapo amesema maendeleo yake yamekuwa ni kupeana migugo kwa wakazi na kusahau sekta muhimu kwa wakazi wa kaunti hii.