SENETA WA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI AMUIMIZA SPIKA WA BUNGE LA POKOT KUFANYA KAZI YAKE NA KUTORUHUSU KUSHAWISHIWA NA UONGOZI WA SERKALI YA POKOT



Seneta wa kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Poghisio ameibua maswali kuhusu jinsi spika wa bunge la kaunti hii Catherine Mukenyang alivyoruhusiwa kurejelea majukumu yake katika bunge hilo licha ya bunge hilo awali kudaiwa kuapa kutomruhusu kurejea.
Aidha kulidaiwa kuwepo tofauti baina ya gavana wa kaunti hii John Lonyangapuo na spika Mukenyang huku spika huyo akidai tofauti baina yao zinatokana na hatua yake kutoruhusu matumizi mabaya ya fedha za bunge hilo hatua iliyochangia kubanduliwa kwake kabla yake kuelekea mahakamani.
Japo akikiri ni haki yake kurejelea majukumu katika bunge hilo, Poghisio amedai kuwa huenda hatua hii ni moja ya mikakati ya gavana Lonyangapuo kutafuta jinsi ya kupata fedha kutoka katika hazina ya bunge la kaunti kwa matumizi ya serikali yake ikizingatiwa sasa ni wakati anapohitaji zaidi fedha hizo.
Poghisio amemtaka spika Mukenyang kutekeleza majukumu yake kwa uwazi na kutokubali kutumika uongozi wa serikali ya kaunti hii kuruhusu mianya ya kufujwa fedha za umma kwani tayari serikali ya kaunti haina rekodi nzuri ya matumizi ya fedha.