SENETA POGHISIO APONGEZA WAWAKILISHI WADI WA POKOT MAGHARIBI KWA KUPASISHA MSWADA WA BBI


Seneta wa kaunti hii ya Pokot Magharibi Samwel Poghisio amepongeza wabunge katika bunge la kaunti hii kwa hatua ya kupitisha mswada wa marekebisho ya katiba wa mwaka 2020.
Akizungumza baada ya kupitishwa mswada huo, Poghisio amesema hatua hiyo imeletea kaunti hii sifa njema huku akiwasuta baadhi ya viongozi katika kaunti hii anaodai kuwa walilenga kuwahonga wawakilishi wadi ili kuuwangusha mswada huo.
Aidha Poghisio amewatetea waakilishi wadi hao kufuatia shutuma za wanaopinga mswada huo, akisema kuwa walichukua muda wao kutafuta maoni kutoka kwa wakazi maeneo mbali mbali ya kaunti hii kabla ya kuupitisha.
Wakati uo huo Poghisio ametoa wito kwa wakazi wa kaunti hii kuunga mkono kikamilifu mswada huo utakapofika hatua ya kura ya maoni akisema BBI italeta manufaa makubwa kwa kaunti hii kimaendeleo kutokana na kiwango cha fedha itakachotengewa.