SENETA DKT SAMUEl POGHISIO APONGEZA MKUTANO WA AMANI ULIOFANYIKA BARINGO


Seneta wa kaunti hii ya Pokot Magharibi Dkt Samuel Poghisio amepongeza mkutano wa amani ambao umefanyika katika hoteli moja kule Baringo ya kusini kati ya maafisa wakuu wa usalama wakiongozwa na mshirikishi wa utawala wa kanda la bonde la ufa George Natembea.
Viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo ni kamishana wa kaunti ya Baringo Henry Wafula pamoja na viongozi mbalimbali wa kaunti hiyo na pia viongozi wa kaunti hii ya Pokot Magharibi akiwamo gavana Pro John Lonyangapuo, Seneta Dkt Samuel Poghisio, spika wa bunge la kaunti Catherine Mukenyang, mbunge wa Pokot Kusini David Pkosing na mbunge wa Sigor Peter Lochakapong.
Mkutano huo ulijiri saa chache tu baada ya serikali kupitia waziri wa usalama wa ndani Dr. Fred Matiang’i kuondoa marufuku ya kutokuwa nje uliokuwa umewekwa baina ya saa kumi na mbili joni hadi saa kumi na mbili alfjiri kufuatia uhasama wa kijamii katika mpaka wa Kapedo na Tiaty.
Akizungumza na kituo hiki Dkt Poghisio hata hivyo amepongeza hatua hiyo ya serikali akisema kuwa itatoa nafasi mwafaka ya kutafuta suluhu la kudumu.