SEKTA YA UCHUKUZI YASALIA KUWA CHANGAMOTO UASIN GISHU


Muungano wa makanisa katika kaunti ya Uasin Gishu imesema kuwa sekta ya uchukuzi ya umma imesalia kuwa changamoto msimu huu wa krismasi kutokana na kuendelea kupuunzwa kwa kanununi zilizowekwa na wizara ya afya katika juhudi za kuzuia masambao wa homa ya Korona.
Sheikh Abubakar Bini ambaye ni naibu wa baraza hilo na katibu wa baraza hilo kaunti ya Uasin Gishu askofu Julius Atsango wamesema kuwa kando na kubeba abiria kupita kiasi abiria hawavalii barakoa na pia matatu hizo hazina vieuzi.
Sheria hizo pia zimeendelea kuvunjwa na wahudumu wa boda boda ambao wanabeba watu zaidi ya mmoja ambao kamwe hawavalii barakoa.
Wawili hao wameonya kuwa kanuni hizo vile vile zimeendelea kupuuzwa katika hafla za harusi na mazishi.
Hali wanayosema huenda ikachangia ongezeko la maambukizi ya Korona msimu huu. Aidha viongozi hao wameitaka serikali kushughulikia kwa upesi matakwa ya wahudumu wa afya wanaoendelea kugoma kote nchini.