SEKTA YA BODABODA YAPUNGUZIWA USHURU POKOT MAGHARIBI.


Wahudumu wa boda boda katika kaunti hii ya Pokot magharibi wamepata afueni baada ya serikali ya kaunti kuwapunguzia ushuru wanaolipa kutoka shilingi 300 hadi shilingi 200.
Akitoa tangazo hilo gavana John Lonyangapuo amewahimiza wahudumu hao kutumia fursa hii ambapo wamepunguziwa ushuru kushirikiana na maafisa wa kukusanya ushuru kwa kulipa kwa wakati na kuepuka mivutano na maafisa hao.
Wakati uo huo gavana Longapuo ametumia fursa hiyo kuwaonya wahudumu hao dhidi ya kutumiwa na wanasiasa kuzua vurugu hasa wakati huu ambapo siasa za uchaguzi mkuu wa mwaka ujao wa 2022 zinatarajiwa kushika kasi.