SEKTA YA BODA BODA YAANDAA UCHAGUZI KAPENGURIA POKOT MAGHARIBI.


Wahudumu wa boda boda eneo la Kapenguria katika kaunti hii ya Pokot magharibi wanaandaa leo uchaguzi wa viongozi wao.
Ni shughuli inayoandaliwa katika uwanja wa michezo wa Makutano huku wito ukitolewa kwa wahudumu hao kujitokeza mapema na kwa wingi ili kuhakikisha shughuli hiyo inaandaliwa na kukamilika kwa wakati.
Aidha miito imetolewa kwa wahudumu hao kutekeleza shughuli hiyo kwa amani, watakaoshindwa katika uchaguzi huo wakitakiwa kukubali matokeo ili kusishuhudiwe migawanyiko miongoni mwa wahudumu hao.