SAFARI LINK YAREJELEA SAFARI ZA NDEGE KATIKA UWANJA WA NDEGE KITALE.
Shirika la safari za Ndege Safari link, limezindua safari zake katika uwanja wa ndege wa Kitale baada ya miaka miwili ya kukatizwa kwa safari hizo kutokana na ukarabati wa uwanja huo kwa kima cha shilingi milioni 221.
Akihutubu kwenye hafla hiyo kamishana Kaunti ya TransNzoia Sam Ojwanga amepongeza hatu hiyo akisema itasaidia kupunguzia wenyeji gharama ya kusafiri hadi Mjini Eldoret ili kupata usafiri wa Ndege, mbali na kufungua uchumi wa maeneo haya na mataifa jirani.
Mkurugenzi mkuu wa Safari link Alex Avedi amesema shirika hilo litakuwa na usafiri wa Ndege mara tano kwa wiki akisema kutokana na hitaji la wasafiri eneo hili watahakikisha kuna Ndege mbili kila siku za kusafirisha abiria hivi karibuni.
Kwa upnde wake Seneta wa Kaunti ya Trans- Nzoia Dkt Michael Mbito amesifia hatua ya serikali kukarabati uwanja huo akiongeza kuwa itaimarisha usafiri na utalii maeneo haya, akikariri haja ya mashauriano miongoni mwa viongozi Kaunti hiyo ili kupatikana kwa ardhi ya upanuzi zaidi wa uwanja huo.