RUTO ATETEA USHINDI WAKE MAHAKAMANI ALHAMISI.
Vikao vya kusikiliza kesi ya kupinga ushindi wa rais mteule William Ruto vinaingia leo siku ya pili baada ya kuaza rasmi hiyo jana.
Leo ni zamu ya mawakili wa Ruto na tume ya uchaguzi IEBC kujibu yaliyoibuliwa katika vikao vya jana pamoja na kutetea ushindi wa Ruto.
Hapo jana maswala makuu yaliibuliwa na mawakili wa mlalamishi mkuu kinara wa chama cha azimio la umoja one Kenya Raila Odinga na mgombea mwenza wake Martha Karua wakishinikiza kutupiliwa mbali ushindi wa Ruto kwani asilimia 50 na kura moja haikuafikiwa katika kutangaza mshindi wa urais.
Aidha mawakili hao walidai kwamba Raila alipunguziwa kura kwenye baadhi ya maeneo na kuongezewa Ruto.
Wakili Julie Soweto alidai kwamba kulikuwa na tofauti ya kura zilizotangazwa katika baadhi ya vituo vya kupigia kura na zilizonakiliwa katika fomu 34a na kuwekwa katika mtandao wa IEBC huku fomu nyingine za IEBC zikizosa nembo za usalama.
Alivitaja vituo 41 ambavyo matokeo yake yana kasoro miongoni mwavio vikiwa katika eneo la Bomet kiambu na kakamega.
Aidha mawakili hao walidai kwamba watu wasio maafisa wa IEBC waliruhusiwa kuingilia teknolojia ya tume hiyo na kisha kuidhinishwa kushughulikia fomu hizo.
Swala la kukamatwa raia watatu wa venezuela pia liliibuliwa katika vikao vya jana ambapo wakili Philip Murgor alidai yaliyobainishwa na maafisa wa upelelezi baada ya kukamatwa kwao yanastahili kupewa uzito unaostahili wakati kesi itakapoamuliwa.