RUTO ATAKIWA KUFANYA MAPATANO NA WAKOSOAJI WAKE


Rais mteule William Ruto ameendelea kupokea shinikizo za kufanya mapatano na viongozi waliokuwa wakosoaji wake wakumbwa katika kipindi ambacho alikuwa akihudumu kama naibu rais.
Tom Juma ambaye ni mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu katika kaunti ya Trans nzoia ameelezea haja ya viongozi mbali mbali kuzika tofauti zao ili kuhakikisha huduma bora pamoja na kudumisha umoja miongoni mwa wakenya.
‘’Ningependa kumhimiza mheshimiwa rais William Ruto tafadhali wewe ni mkristo na miaka yote tmekuona ukienda kanisani na kuwambia watu kwamba tumweke Mwenyezi Mungu mbele, tafadhali usilipoize kisasi kwa wale ambao walikuwa wakikuzungumzia vibaya.” Amesema Juma.
Aidha juma amewarai wakenya kudumisha amani hata baada ya uchaguzi huo.
“kwa hivyo mimi ningependa kuwahimiza wakenya haya mambo ya kupigana tulichoka nayo. Sisi saa hizi tusonge mbele kwa sababu hata ukienda kupigana haitaleta unga kwa meza yako.” Amesema.
Ikumbukwe tayari Ruto ameashiria utayarifu wake kushirikiana na viongozi wote baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kinyang’anyiro cha urais.