RUTO ASUTWA KWA KUINGILIA UBUNGE WA SABOTI TRANS NZOIA.

Mbunge wa Saboti kaunti ya Trans nzoia Caleb Amisi amemsuta naibu Rais William Ruto kwa kile amedai kupanga jinsi atahakikisha anabanduliwa katika kiti hicho kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi agosti mwaka huu.
Amisi amemtaka Ruto kushughulika na siasa za kitaifa kwa kuwaeleza wakenya jinsi ambavyo atashughulikia hali ya uchumi ambayo imezorota pakubwa nchini na kuacha kujihusisha na siasa za chini kama vile za maeneo bunge.
Amisi alikuwa akimjibu Ruto ambaye aliwataka wenyeji eneo bunge la Saboti kuhakikisha wanamuondoa maamlakani mwezi agosti wakati alipozuru kaunti hiyo katika misururu ya mikutano ya kiuchumi ulioandaliwa mjini Kitale.

[wp_radio_player]