RUTO ALAUMIWA KWA TOFAUTI ZINAZOSHUHUDIWA BAINA YAKE NA RAIS UHURU KENYATTA


Tofauti baina ya rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto zikiendelea kushuhudiwa, wadau mbali mbalimbali wameendelea kulaumu upande wa naibu rais kwa mizozo baina ya wawili hao.
Akizungumza na wanahabari mjini Makutano kaunti ya Pokot Magharibi, wakili Philip Magal amesema Ruto ameendelea kumkosea heshima rais Kenyatta kupitia wandani wake licha yake mwenyewe kudai kumuunga mkono rais.
Licha ya tofauti ambazo zinashuhudiwa kati yao Magal aidha amefutilia mbali uwezekano wa wawili hao kutengana kabla ya mwaka 2022.