RIPOTI YA MCHUJO WA MAWAZIRI TRANS NZOIA YATARAJIWA BUNGENI.


Kamati ya uteuzi katika kaunti ya Trans nzoia inatarajiwa kuwasilisha ripoti yake bungeni baada kukamilisha kuandaa ripoti ya mawaziri wateule iliyowahoji juma lililopita.
Baada ya kuiwasilisha ripoti hiyo wawakilishi wadi thelathini na watatu watapata fursa ya kuijadili na kupigia ripoti hiyo kura kuidhinisha majina yote kumi na mmoja ama kuyakataa.
Wakati wa mahojiano baadhi ya mawaziri wateule walishindwa kuyataja majina ya machifu wa kata wanayotoka wakati walipokuwa wakiwekwa mizani.
Mchanganuzi wa siasa katika eneo hilo kipyego some alisema kwamba kuna uwezekano mkubwa kwamba bunge hilo litaidhinisha majina hayo yote na kumpa fursa gavana wa kaunti hiyo George Natembeya kuanza kazi kutekeleza miradi aliyo nayo.
Waliokuwa wameteuliwa ni kamishna wa kaunti ya Busia Samson Ojwang kuwa waziri wa utumishi wa umma Janerose Muthama kuwa waziri mteule wa ardhi ujenzi mipango ya miji Julia kichwen miongoni mwa wengine.