RAMANI YA MAHAKAMA KUU YA KAPENGURIA YATAJWA KUWA BORA.
Msajili mkuu wa mahakama humu nchini, hakimu Ann Amadi, ameisifia ramani ya ujenzi wa mahakama kuu ya Kapenguria kaunti hii ya Pokot magharibi kwa kuwa na vitengo tofauti ambavyo vitashughulikia wateja mbalimbali.
Amesema katika mahakama hiyo kuna maeneo ya kuhudumia watu waliona changamoto za kimaumbile, akina mama wanaonyonyesha pamoja na watoto wanaotafuta huduma za mahakama miongoni mwa mengine.
Kwa upande wake hakimu mkuu katika mahakama kuu ya kitale luka kimaru, amethibithisha kuwa kuna kesi nyingi ambazo hazijaamuliwa katika mahakama hiyo, huku nyingi ya kesi hizo zikitoka katika wadi ya alale katika eneo bunge la kacheliba kauti hii ya pokot magharibi.
Ni kauli ambayo imeungwa mkono na kamishna wa kaunti hii Apolo Okelo ambaye ameiomba huduma hiyo kuSambazwa hadi kaunti ndogo ya sigor ili wakenya wapate huduma hizo kwa karibu.