RAIS KENYATTA ASHAURIWA KUWEKA WAZI SABABU ZA KUWATEMA NJE MAJAJI 6 WA MAHAKAMA YA UPEO

Siku chache baada ya Rais Uhuru Kenyatta kukosa kuwateua majaji 6 wa mahakama ya upeo shinikizo zinazidi kutolewa kwa Rais Uhuru Kenyatta kutoa wazi sababu zilizo pelekea majaji hao kukosa kuteuliwa na kuapishwa.
Akihutubu baada ya kuhudhuria ibada ya jumapili katika kanisa la AIC Lessos, Mshauri wa kisheria katika afisi ya Naibu wa Rais Dkt Abraham Singoei ametaja hatua ya Rais kuwa ukiukaji wa sheria akisema hatua hiyo ni tisho kwa taifa haswa linapojiandaa kwa uchaguzi mkuu wa 2022.
Aidha Dkt Singoei ametoa wito kwa taasisi zote za serikali pamoja na watumishi wa umma kuhakikisha wanafuata na kutetea katiba kwa kuhakikisha kuwa kila jambo wanalotekeleza ni kwa mujibu wa katiba na sheria za taifa hili.