RAIS KENYATTA ASHAURIWA KUKAMILISHA MIRADI ALIYOAHIDI KATIKA KAUNTI YA BUSIA


Siku chache tu baada ya rais Uhuru Kenyatta kukutana na wabunge wa Mlima Kenya baadhi ya viongozi wa eneo la magharibi sasa wanamtaka Rais Uhuru Kenyatta kuanzisha ama kukamilisha miradi aliyoahidi eneo hilo wakati wa kampeini za mwaka wa alfu mbili kumi na tatu na mwaka wa alfu mbili kumi na saba.
Viongozi hao wakiwemo wabunge John Bunyasi wa Nambale, Joseph Oyula wa Butula na gavana wa kaunti ya Busia Sospeter Ojamong wamesema kwamba miradi iliyopendekezwa na serkali ya jubilee mingi haijatekelezwa.