RAIS ATAKIWA KUZURU BONDE LA KERIO KUANGAZIA SWALA LA USALAMA.
Baadhi ya viongozi katika kaunti ya Elgeyo marakwet wamemtaka rais Uhuru Kenyatta kuzuru bonde la kerio ili kuweka mikakati thabiti itakayosaidia katika kutatua utovu wa usalama katika kaunti hiyo.
Wakiongozwa na mbunge wa Keiyo kusini Daniel Rono wamesema kuwa pana haja ya hatua za dharura kuchukuliwa ili kuthibiti hali baada ya kushuhudiwa kwa mashambulizi ya mara kwa mara katika mipaka ya kaunti hiyo na ile ya Baringo.
Rono aidha amewasuta viongozi wakuu wa wizara ya usalama nchini kwa kuzembea katika majukumu yao akitaka waachishwe kazi.
Ni kauli ambayo pia imetolewa na mwanasiasa Mika Kigen akisema rais Kenyatta ndiye mwenye uwezo wa kukabili tatizo hilo kauli ambayo imeungwa mkono na wazee ambao wamelalamikia mauaji ya kila mara eneo hilo.