RAIS ATAKIWA KUSHUGHULIKIA SWALA LA MASKWATA TRANS NZOIA.
Rais Uhuru Kenyatta anapotarajiwa kuzuru eneo la bonde la ufa, wakazi wa kaunti ya Trans nzoia wamemwomba kuangazia tatizo la maskwota na unyakuzi wa ardhi zilizotengewa taasisi za elimu miongoni mwa mengine.
Kulingana na aliyekuwa mwakilishi wadi ya Chepchoina George Masika, wakazi wengi ambao wazazi wao walifanya kazi katika shamba la shirika la ustawishaji kilimo ADC ni maskwota na wanaishi katika lindi la umasikini.
Aidha katibu mkuu wa chama cha ushirika cha wafanyibiashara katika eneo la Swam kwenye mpaka wa Kenya na Uganda Daniel Sapiri, amemwomba rais Kenyatta kuagiza kuchapishwa katika gazeti rasmi la serikali kipande cha ardhi katika eneo hilo ili kutumika kuwa kituo cha forodha na kujengwa soko.