RAIS ATAKIWA KUONDOA KAFYU SHULE ZINAPOFUNGULIWA RASMI.


Wazazi katika kaunti ya Trans nzoia wamewaomba walimu wakuu kuzingatia agizo la waziri wa elimu prof. George Magoha la kutowatuma nyumbani wanafunzi kufuatia ukosefu wa karo.
Wazazi hao wamesema kuwa wamepitia changamoto nyingi katika kipindi hiki cha corona, na pia kipindi ambacho wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la nane KCPE na wale wa gredi ya nne wamekuwa nyumbani na sasa ni wakati wanafaa kusalia shuleni.
Aidha wazazi hao wamemtaka rais Uhuru Kenyatta kuondoa agizo la kutokuwa nje kuanzia saa moja usiku hadi saa kumi alfajiri kwa kaunti zilizowekewa mashariti hayo ili kuwawezesha wanafunzi wanaosomea shule za mbali kusafiri.