RAIS ATAKIWA KUOMBA MSAMAHA KUFUATIA GHARAMA YA JUU YA MAISHA.


Kinara wa chama cha FORD Kenya Moses Wentangula amemtaka Rais Uhuru Kenyatta kuwaomba wakenya Msamaha kutokana na gharama ya juu ya maisha swala analosema limetokana na serikali kutotilia maanani maswala muhimu yanayomgusa mwananchi wa kawaida. 

Akihutubu mjini Kitale kwenye kampeni za muungamo wa Kenya Kwanza Wetangula ambaye pia ni Seneta wa Bungoma amemtaka Rais kutojihusisha na siasa na urithi wake na badala yake kushughulikia mahitaji ya wakenya haswa kupanda kwa gharama ya maisha.

Aidha Wetangula amemtaka mwenyekiti wa tume ya uwiano na utangamano NCIC Samwel Kobia kukoma kutoa vitisho dhidi ya kampuni ya facebook akishutumu kauli ya kudhibiti mtandao huo wakati wa uchaguzi.
Wakati uo huo mbunge wa Endebess Dkt Robert Pukose amekosoa hatua ya Kamishna wa Kaunti ya Trans Nzoia Sam Ojwang kwa kuwashurutisha maafisa wa  utawala kujihusisha na kampeni za muungano wa azimio la umoja akisema ni kinyume cha sheria kwa watumishi wa umma.